Wednesday, November 18, 2015

PSPF KWA KUSHIRIKIANA NA NHIF YAANZISHA HUDUMA YA “FAO LA MATIBABU LA MFUKO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA PSPF”

1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF Michael Mhando kulia na Mkurugenzi wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakitiliana saini mkataba wa bima ya afya kwa wana Vikundi wa Mfuko huo katika huduma ya “Fao la Matibabu la Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF” uliozinduliwa leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Maofisa mbalimbali wa mifuko hiyo pamoja na wanufaika ambapo baadhi ya wanufaika walikabidhiwa kadi zao za uanachama , Katikati  ni Omary Khalfan Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA pamoja na maofisa wa mashirika hayo wakishuhudia tukio hilo.
2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF Michael Mhando kulia na Mkurugenzi wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakibadilishana nyaraka za kmataba huo mara baada ya kusaini kwenye uzinduzi huo.
3
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF Michael Mhando kulia na Mkurugenzi wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakikata utepe kuzindua rasmi huduma hiyo kulia ni Omary Khalfan Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.
4
Bw Omary Khalfan akikimkabidhi kadi ya uanachama Eliaichi Makundi  mnufaika wa huduma hiyo inayotolewa na  PSPF na NHIF.
5
Bw Omary Khalfan akikimkabidhi kadi ya uanachama Bakari Mbilambi   mnufaika wa huduma hiyo
6
Bw. Omary Khalfan akikimkabidhi kadi ya uanachama Anna Mkunda   mnufaika wa huduma hiyo.
7
Bw Omary Khalfan akikimkabidhi kadi ya uanachama Salim Madenge mnufaika wa huduma hiyo.
8
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF Michael Mhando akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo wa huduma ya Bima ya Afya kwa wanachama wa wajasiriamali wa PSPF.
9
Baadhi ya maofisa kutoka mfuko wa PSPF wakiwa katika hafla hiyo.
10
Baadhi ya maofisa kutoka mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF wakishuhudia utiaji saini mkataba huo.
11
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akitoa hotuba yake wakati wa utiaji saini wa mkataba huo katika ya NHIF na PSPF.
Post a Comment