Baadhi ya Nyumba zikibomolewa mapema leo mchana mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni,ambapo zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo. Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, imekusudia kuanza kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
Baadhi ya wakaazi wa mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni wakishuhudia bomoa bomoa inayofanyika leo katika manispaa hiyo maeneo mbali mbali ambapo Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
Moja ya Nyumba iliyojengwa eneo la wazi katika mtaa wa Bwawani ikibomolewa
Askari jeshi la polisi wakihakikisha suala la usalama katika tukio hilo
Ubomoaji wa nyumba ukiendelea eneo la Manispaa ya Kinondoni
TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA KUHUSIANA NA UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI
Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.
Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
a) Bila kibali cha ujenzi
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.
Comments