Monday, November 09, 2015

SAFARI TA MWISHO YA MAREHEMU PASCHAL EUGENE ZIMBATIS

Pichani Mzee Paschal Eugen, aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), enzi za Uhai wake, Marehemu Paschal alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam, amelitumikia Shirika la Nyumba la Taifa kwa muda mrefu kwa utumishi uliyo na uadilifu. Mazishi yake yamefanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo.

Marehemu Paschal Eugen aliyekuwa akifanyia kazi NHC Mara alikuwa akiendelea na matibabu yake jijini Dar-es-salaam katika hospital ya Regency alifariki dunia saa 10.30 alfajiri ya Ijumaa.

Marehemu alikuwa akisumbuliawa na tatizo la sukari lililomsababishia madhara ya kutopona kidonda, kufeli kwa figo na Shinikizo la Damu iliyoathiri mfumo wa fahamu. Mipango ya mazishi ilikuwa ikifanyika nyumbani kwake eneo la Mburahati Motomoto na baadaye maziko Msata.

Mwenyenzi Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 Ndugu jamaa na marafiki waliohudhuria kwenye Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Paschal kwenye Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.

 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa, mkoa wa Mara, Frank Mambo akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Paschal kwenye Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.
 Ndugu wa Marehemu Paschal akisoma wasifu wa marehemu kwenye Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuatilia taratibu za mazishi ya Paschal wakati wa Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi.

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu  akitoa neno wakati wa Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani. 

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu  akitoa neno wakati wa Mazishi ya Marehemu yaliyofanyika juzi kijijini kwao Msata, Bagamoyo mkoani Pwani. 
Post a Comment