Sunday, November 08, 2015

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)LATOA KIBALI KWA TAASISI YA UHASIBU (TIA) MBEYA KUANZISHA KOZI NYINGINE ZA SHAHADA YA MASOKO


Kikosi cha brasband cha Magereza kikiongoza Maandamao kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo ya Kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya .

Baadhi ya wahadhiri wa Taasisi hiyo ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya wakiandamana kuelekea uwanjani tayari kwa mahafali hayo .
Wahitimu wakiwa katika maandamano hayo ya Mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa Kampasi ya Mbeya.
Meza kuu wakipokea maandamano ya wahitimu katika mahafali ya kumi na tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Chuo hicho jijini Mbeya.
Baadhi ya wahitimu wa Uhasibu  (TIA) kampasi ya Mbeya
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt .Joseph Kihanda akizungumza kwenye mahafali ya Kumi na tatu ya Taasisi na ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya .
Mgeni rasmi Ndugu Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye pia alimwakilisha Waziri wa Fedha katika mahafali hayo ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya.
Wahitimu wa Masomo ya Uhasibu Katika Taasisi hiyo wakisikiliza kwa umakini nasaha kutoka kwa mgeni rasmi .
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Ilemi jijini Mbeya kikitoa burudani katika mahafali hayo .
Mgeni rasmi Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akitoa zawadi kwa washindi walio fanya vyema katika masomo yao.
Baadhi ya wahitimu wa masomo ya Uhasibu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Kampasi ya Mbeya wakitunukiwa rasmi cheti cha awali,Stashahada na Shahada ya Uzamili katika fani mbalimbali ambapo jumla ya wanafunzi 1689 wamehitimu mafunzo hayo ambapo kati yao wanaume ni 838 na wasichana 851 .

Baraza la Taifa la
Elimu ya ufundi (NACTE)limetoa kibali kwa taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
kampasi ya Mbeya ili kuongeza kozi nyingine za shahada ya Masoko na uhusiano
kwa umma (Bachelor Degree in Marketing and public Relation kwa mwaka wa masomo
wa 2015-16.
        Aidha baraza hilo pia limetoa kibali kwa kuanzishwa kwa kozi nyingine ya shahadaya
uhasibu wa fedha za umma (Bachelor Degree in Public Sector Accounting and
Finance) kwa mwaka huu wa masomo.
 Kauli
hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt.Joseph
Kihanda kwenye mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi na y a tatu kufanyika katika
kampasi ya Mbeya.
        Amesema katika mwaka wa masomo wa
2014-2015 kufuatia maombi ya muda mrefu ya wadau wake kampasi ya mbeya ilianza
kutoa kozi za shahada ya uhasibu na shahada ya Ununuzi na Ugavi ambazo mwitikio
wake umekuwa mkubwa hivyo kulazimika kuomba kibali cha kuanzisha kozi nyingine
ambazo tayari baraza hilo limekwisha toa kibali .
        Amesema kuanzishwa kwa kozi hizo
kumeiwezesha kampasi ya Mbeya kuwabakiza wanafunzi wanaohitimu kozi za
Stashahada katika fani husika ambao hapo awali walilazimika kuhamia vyuo vingine
vinavyotoa kozi hizo kwenye ngazi ya shahada na hivyo kuikosesha Taasisi
mapato.
        Aidha Dkt Kihanda amesema kuwa kuanza kwa
kozi hizo  pia kutawawezesha wakazi wa mbeya na mikoa mingine ya jirani
kupata fursa ya kujiendeleza kitaaluma Katika ngazi ya  shahada kwani
masomo yanatolewa katika mfumo wa kutwa na jioni hivyo kukidhi kiu ya wengi.
        Hata hivyo amesema kampasi ya mbeya
imejiimarisha sana katika utoaji wa elimu yenye ubora ili kuwawezesha wahitimu
kufanya vizuri katika masomo yao ya baadae na katika sehemu zao za kazi.
            Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya wizara ya fedha Profesa Isaya
Jairo amesema bodi hiyo itashirikiana na uongozi wa TAASISI  kuishauri
wizara ya fedha kuitngea fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali
pamoja na vitendea kazi.
Katika
mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 1689 wa stashahada na stashahada za udhamili
katika fani mbalimbali wanahitimu masomo yao ambapo kati yao wasichana 851 na
wanaume 838.
(Imeandaliwa na
Emanuel Madafa Jamiimojablogu Mbeya)

No comments: