Thursday, November 19, 2015

JINA LA WAZIRI MKUU MTEULE MHE. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA LILIPOWASILISHWA BUNGENI DODOMA LEO


 Mpambe wa Rais Kanali Mkeremi akiingia bungeni mjini Dodoma leo asubuhi akiwa na bahasha yenye jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa  na  Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
  Mpambe wa Rais Kanali Mkeremi akimkabidhi Spika Job Ndugai bahasha yenye jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa  na  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
 Spika Job Ndugai akiinua bahasha kabla ya kusoma  jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa bungeni  na  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
 Wakati hayo yakiendelea ndani ya bunge Mbunge wa Rwangwa Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili viwanja vya bunge akiwa peke yake bila shaka akiwa hana habari kwani usiri wa kupatikana na hatimaye kuwasilishwa jina la Waziri Mkuu Mteule ulikuwa mkubwa sana.
 Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa na hatimaye kupigiwa kura na kupita kwa kishindo kwa kura 258 ama asilimia 73.5 ya idadi ya kura zilizopigwa.
Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa
 Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimtanguliza  Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia nafasi hiyo, akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani aliyoonesha juu yake, anawashukuru pia wabunge kwa kumpa kura nyingi, na wapiga kura wake kwa kumchagua tena na kumuwezesha kufika hapo. Picha na Sultani Kipingo

No comments: