Sunday, November 15, 2015

WAKATAA KUPANDISHWA KWA BEI ZA MAJI


 Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya akiwa anasoma garama mpya ambapo zilipendekezwa kuongezwa na changamoto walizonazo
 Mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wa pili kulia  akiwa na baadhi ya viongozi  waliokaa meza kuu
 picha juu na chini wananchi waliouthuria katika mkutano huo


mmoja wa wananchi  aliyejitambulisha kwa jina la  Ayubu
Mshote akichangia mada
mwananchi wa kata ya sombetini Jenifa Sumaye akiwa anachangia mada wakati  mkutano wa wadau na watumia wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati namaji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho ukiendelea 

 Na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wa jiji la Arusha wamekataa kupandishwa kwa gharama za maji kutokana na kutokuwa na kutokupatiwa huduma bora ya maji na mamlaka ya
maji safi na maji taka(AUWSA) ya jiji hili.

Hayo waliyasema jana jiji hapa wakati wa mkutano wa wadau na watumia wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati na maji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho jijini hapa.

Walisema kuwa hawawezi kukubali mamlaka ya maji safi na maji taka kupandisha gharama za maji wakati huduma ambazo wanazitoa sio nzuri na
hadhikithi maitaji ya wananchi .

Kwa upande wa mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ayubu Mshote alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikipata faida kila mwaka lakini wameshindwa kuboresha miundo mbinu yake hali inayofanya kuwepo kwa tatizo la maji pamoja na upotevu wa maji .

Alisema kuwa faida wanayopata AUWSA ikitumika vyema kwa mahesabu inaweza kugharamia shuhuli za uendeshaji na uwekezaji  na pia itasaidia kuweza kubuni vyanzo vipya vya maji vitakavyosaidia kuboresha huduma za maji na kumfikia kila mwananchi .

Naye Jenifa Sumaye alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana la maji katika jiji hili hali ambayo inawafanya wananchi kununua maji kwa bei ghali ,na pia aliitupia mamlaka hiyo ya maji lawana na kusema kuwa wamekuwa wanakata maji kwa kipindi kirufu halafu wanakuja kusoma mita na kutoa bili ambayo sio ya kweli.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa baraza la ushauri na watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC) Mubezi Lutaihwa alisema kuwa wao hawajaunga mkono upandishwaji wa bei za huduma ya maji kwani mamlaka hiyo ingebana matumizi na kuongeza ufanisi  katika kutoa huduma na sio kuwapandishia wananchi gharama.

Alisema kutokana na histori ya upatikanaji wa faida wa AUWSA baraza alioni kama kunasababu yeyote ya kupandisha bei ya huduma kwa sasa kwani faida inayopatika inatosha kugaramia shuhuli za uendeshaji na uwekezaji.

Kwa upande wa mkurugenzi wa AUWSA Eng. Ruth koya alisema  wao wameamua kupendekeza kupandishwa kwa gharama za maji ili kuweza  kutoa huduma bora na kuweza kukarabati miundo mbinu ya maji.

“Tunapandisha gharama hizi ili kuweza kutoa huduma bora pamoja na pia kwa tumepandisha ili kuweza  kupata hela ya kutatua changamoto mbalimbali kwani kwa sasa tumeondolew msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani na sasa hivi tunalipia asilimia yote mia moja na pia garama za umeme zimezidi hivyo tunaongeza ili tuweza kutatua matatizo hayo”alisema koya Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa EWURA Nzinyangwa Nchani alisema kuwa wamepokea maoni kwa ujumla watayafanyia uchambuzi wa kina na kuona pendekezo lipi linafaa au kitu gani kifanyike na pia watapitia historia ya mamlaka hiyo na watatoa maamuzi ili wananchi waendelee kupata huduma bora.

No comments: