Friday, November 06, 2015

WABUNGE VITI MAALUM CCM YAPATA 64, CHADEMA -36, NA CUF- 10


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza idadi ya wabunge wa viti maalumu ambao vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vimepata baada ya kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge nchi nzima.
Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema chama cha CCM ambacho kilipata jumla ya kura milioni 8.3 kimepata wabunge 64 wakati chama cha CHADEMA ambacho kilipata kura milioni 4.7 kimepata wabunge 36
CUF iliyopata kura milioni 1.2 kimepata wabunge 10, na kuainisha kuwa jumla ya wabunge wa viti maalumu vya ubunge ni viti 113 wakati viti vitano vitatoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar. SOURCE:EATV.

No comments:

RAIS NDAITWAH AONDOKA BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TATU NCHINI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Dkt, Netumbo...