KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA POLISI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments