Wednesday, November 11, 2015

TRA YAJIVUNIA KASI KATIKA UKUSANYAJI KODI.

ISO 9001:2008 CERTIFIED

TAARIFA YA MAKUSANYO YA KODI.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi  trililion 3, 778,097.5 kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na asilimia  97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3, 872,337.4 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao unaitaka kukusanya Ths . Trililioni 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kwa mujibu wa Kamishna  Mkuu wa TRA Rished Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9 ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 854,922.9.

Mwezi Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni1,067,888.3 zilikusanywa ikiwa ni asilima 91.7 ya lengo trilioni 1,163,999.4 kwa mwezi mwezi Oktoba TRA  iilkusanya shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 976,441.5.

Taarifa ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu ya TRA” amesema Bw. Bade.

Mafanikio katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.

Wito wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.

Sambamba na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”

Rished Bade
KAMISHNA MKUU

No comments: