Thursday, November 19, 2015

Aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL na wenzake 2 wakutwa na hatia

kisutu19Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemkuta na hatia aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), Bw. David Mattaka na wenzake wawili baada ya mashahidi 13 kutoa ushahidi wao mahaakamni hapo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Emmilius Mchauru  amesema mahakama imejiridhisha bila shaka baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha mashahidi 13 kuhusu tuhuma zinazomkabili kigogo huyo wa zamani wa ATCL za matumizi mabaya ya ofisi kwa kutanagza zabuni ya ununuzi wa magari yaliyochakaa 26 na kuisababishia hasara serikali ya mabilioni ya shilingi.
Washitakiwa wote watatu wakiongozwa na mawakili wao walikubali kutoa ushahidi wao kwa kula kiapo ambapo mashahidi wa washitakiwa hao wanatarajiwa kuanza kuwatetea mapema Desemba 10 na 11 huku dhamana zao zikiendelea.
Katika shauri hilo la matumizi mabaya ya ofisi linawakabili David Mattaka aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa ATCL na Elsaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani, Wiliam Haji

No comments: