DC PAUL MAKONDA AZINDUA UMOJA WA WATENGENEZAJI KEKI TANZANIA (TCBA)


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kulia) na Mdau wa Keki, Mama Cythia Henjewele (wa pili kushoto), wakikata keki maalumu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Watengeneza keki Tanzania (Tanzania Cake Bakers Association -TCBA), uliofanyika katika Mgahawa wa City Lounge Posta mpya Dar es Salaam jana. Kulia ni Mshehereshaji, Makena na Mdau wa Keki, Philip Mbonde.
 Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza (kushoto), akimlisha keki mgeni rasmi DC Makonda. Katikati ni mdau wa Keki Cythia Henjewele.
 Mtengeneza keki,  Roselins Sia Adhero (kulia), akimkabidhi keki DC Makonda.
 DC Makonda akimlisha keki Cythia Henjewele.
 Watengeneza keki mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
 Ni watengeneza keki wakipigana picha.
 Ni furaha tu kwa watengeneza keki.
 Mshauri wa masuala ya ujasiriamali, Marione Elias akizungumza na wadau hao wa keki.
 DC Makonda akitoa hutuba yake ya uzinduzi. Kutoka kushoto ni mwanzilishi wa umoja huo,  Stellah Rwabutaza, Mdau wa keki, Philip Mbonde na Mdau wa keki, Cythia Henjewele.
 Mdau wa keki Philip Mbonde (kushoto), akimlisha keki mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza. Kulia ni mdau wa keki, Cythia Henjewele.
Ni furaha na shangwe na kupeana keki. “Hapa ni kazi tu”

 Moja ya keki iliyotengenezwa kwa nafaka.
………………………………………………………………………………………………………………
 Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema kazi kubwa ya watengeneza keki hapa si kwa ajili ya kutoa burudani bali inasaidia kuinua uchumi wa nchi.
Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua Umoja wa Watengeneza Keki Tanzania ( (Tanzania Cake Bakers Association -TCBA), hafla iliyofanyika ukumbi wa City Lounge Posta mpya ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Kazi mnayoifanya si kutoa burudani pekee bali mnalisaidia taifa kuinua uchumi kikubwa endeleeni kuwa wabunifu zaidi wa kutengeneza keki za aina mbalimbali” alisema Makonda.
Makonda aliwataka watengeneza keki hao kila mmoja wao kujisogeza zaidi kwa kupanua wigo wa kazi zao kwa kuwa na vyombo vya muziki, kupiga picha za manto na video badala ya kila kazi kufanywa na mtu mwingine.
Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza alisema umesaidia kuwaungani watengeneza keki nchini na wameweza kutambuana na kubadilishana ujuzi.
“Kwakweli umoja huu umetuanganisha sana sisi watengeneza keki jambo litakalosaidia kufanya kazi zetu kwa pamoja” alisema Rwabutaza.
Stellah alisema changamoto kubwa waliyonayo ni kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwakamata mara kwa mara ambapo waliomba watoe maelekezo ya nini wafanye ili kuendeleza kazi yao hiyo.
Mdau wa keki kutoka mkoani Tanga, MC Janeth Mwita alisema umoja huo umewafanya wawe na mtandao wa kutafuta masoko ya keki na kujifunza ubunifu wa kutengeneza keki za aina mbalimbali.

Comments