Friday, November 27, 2015

MRADI WA 'SAFARI SATELLITE CITY' WAPATA MAJI YA KUTOSHA KWA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU 100

Uongozi wa Shirika Mkoa wa Arusha umefanikisha uvutaji wa bomba la maji safi kutoka umbali wa Kilomita1.5 kama sehemu ya kuwezesha mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika mji mdogo wa Safari City kuanza mwaka ni kama ilivyopangwa.
Hatua hiyo muhimu imechukuliwa kutokana na ukosefu wa maji katika eneo hilo la Safari City na gharama kubwa ya kupeleka maji kutoka eneo la mashamba ya Magereza ambapo Shirika linalenga kusukuma zaidi ya lita 3,000,000 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya jiji lote huko baadaye.
Aidha, kiasi cha lita 100,000 ambayo imewekewa hifadhi inatosheleza kabisa kwa malengo ya sasa ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa lengo la kuutangaza mji huo na kuwapeleka wakazi wengi kwa muda mfupi.
Wafanyakazi  wa Shirika ofisi ya Mkoa wa Arusha wakifurahia mafanikio hayo ya maji kufika katika mradi wa Safari City. Kufika kwa maji haya kunaashiria kuanza kwa mradi wa ujenzi wa  nyumba za gharama nafuu ambazo zilikwama kutokana na ukosefu wa maji. 

Wafanyakazi wakipata maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusu matumizi ya maji hayo, ukubwa wa hifadhi hiyo ya maji na uwezo wa kuhudumia zaidi ya nyumba 100 bila tatizo lo lote.  Hifadhi hiyo ni ya lita 100,000 na upo uwezo wa kuongeza maji kila siku kwa karibu lita 60,000.


Wafanyakazi wakikagua kazi kubwa iliofanyika kuhakikisha maji yanayosukumwa yako salama, yanalindwa na yanatumika kwa malengo yaliokusudiwa.
 Maji ya kuendeleza mradi wa Safari City yakizinduliwa rasmi na Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu James Kisarika tarehe 24/11/2015. Jirani wa kwanza kupata maji hayo ni mama  Sophia Rajab.
Picha inamwonyesha inamwonyesha mama Sophia Rajabakisaidiwa kubeba maji yake na Ndugu Kisarika.        
 

Baadhi ya wakina mama wakiwa katika foleni na  ndoo zao wakisubiri kupata maji kwa mara ya kwanza kabla ya uzinduzi. Katika muda usiozidi dakika moja presha ya maji hujaza ndoo ya lita 20.

Bomba la maji yaliyounganishwa na NHC Arusha likitiririsjha maji muda mfupi baada ya kuzinduliwa

No comments: