Wanafunzi wenye mahitaji maalum vyuo vikuu waaswa kutumia vyema utaalamu walioupata kuendesha maisha yao
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga. Picha na Frank Shija, MAELEZO
Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jana.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Balozi Nicholas Kuhanga akiwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) alipokuwa mgeni wa Chuo katika Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu.
Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwa kupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu mara baada ya kupokea zawadi yake ikiwemo kukabidhiwa Cheti chake mbele ya hadhara wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo.
Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwakupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akionyesha Cheti chake cmbele ya hadhara mara baada ya kuwa muhitimu wa kwanza kukabidhiwa cheti wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Mbali na kukabidhiwa Cheti chake cha Shahada papo hapo muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo.
Mgeni rasmi wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu.
………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Prof. Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha Studi za Mawasiliano Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.
Prof. Qorro alisema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.
“Hawa ni wanafunzi wenye uelewa mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo fimbo nyeupe, vifaa vya kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za miguu mitatu, viti maalu na mahitaji mengine ya kijamii” alisema Prof.Qorro.
Prof.Qorro aliongeza kuwa ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi wanapojaza fomu za kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili waandaliwe mahitaji hayo ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili kuwawezesha kuwahi vipindi vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mahafali hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya 8000 na jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu katika mahafali hiyo ya nane.
Naye muhitim wa mwaka wa tatu katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo ya sanaa Andrea Sanga ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum (mlemavu asiyeona) alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana na kuheshimu ratiba kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake binafsi ya kujisomea.
Zaidi ya hayo, Sanga alisema kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na wanafunzi wenzake na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa wakati na kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira yake kuu ya mafanikio
Comments