Saturday, November 07, 2015

WABUNGE WA VITI MAALUM HAWA KUTOKA CCM, CHADEMA NA CUF HAPA


Mwenyekiti  wa Tume ya Taifa ya Uchanguzi  Jaji Msitafu Damian Lubuva  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya majina ya wabunge wa Viti Maalum yatapatikana katika Vyama husika kwa mujibu wa Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama ila Tume (NEC)iweze kufanya Uteuzi, kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Emmanuel Kavishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  Jaji Msitafu Damian Lubuva 
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Viti Maalum vya Wabunge 110 kwa vyama vitatu ambavyo vimevuka asilimia tano ya kura za wabunge.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva amesema idadi ya wabunge imeongezeka kwa kufikia asilimia 40 kutokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 kwa kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake.
Lubuva amesema kutokana na  kuwepo  majimbo ya nane ambayo hayakufanya uchaguzi kunafanya viti vitatu kutokuwepo, baada ya uchaguzi wa majimbo hayo viti vitarudi kwa vyama.
Katika mgawanyo wa viti maalumu vya wanawake katika bunge  linalotarajiwa kuanza hivi karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata viti 64, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) viti maalum 36 na Chama cha Wananchi (CUF)  Viti Maalum 10. 
Majina ya viti maalum yatapatikana  katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa  Tume ya kila chama  ili tume iweze kufanya uteuzi. 

No comments: