Sunday, October 04, 2015

WAHITIMU WA NBAA WAMEASWA KULINDA, KUTUNZA NA KUSIMAMIA VIAPO VYA TAALUMA YAO.

07

Baadhi ya wahitimu wakijiaandaa kabla ya kuanza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
08
Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiongoza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
01
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiongea na wahitimu wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
02
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya kuongea na wahitimu wakati wa mahafali ya 37 wa Bodi hiyo pamoja na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
03
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa hotuba fupi kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
04
Baadhi ya wahitimu wa Bodi NBAA wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 972 walipata CPA na wahitimu 87 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
05
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akimpongeza mmoja wa wahitimu wa CPA aliyefanya vizuri kwenye mitihani yake wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
06
   09
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) na wahitimu CPA wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
..……………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wahitimu wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) ambao ni wataalamu wa masuala ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu wameaswa kulinda, kutunza na kusimamia viapo vyao wakati wakitekeleza majukumu yao ya kihasibu ipasavyo katika sehemu zao za kazi 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya NBAA yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
“Kiapo mlichoapa leo kiwe chachu ya ufanisi katika utendaji wenu wa kazi, kushuka kwa kiwango cha maadili katika utumishi kunatokana na kuota kwa mizizi katika suala la fedha”
Prof. Mwandosya aliendelea kusisitiza, “Mlinzi mkuu wa fedha katika sehemu yeyote ile ni Mhasibu, nanyi leo mnahitimu, mnapaswa kuwa waaminifu kwa familia zenu, taaluma yenu na kwa taifa mkiongozwa na kiapo mlichoapa, isiwe ni sehemu ya ajenda ya leo ya kutimiza wajibu, bali kiapo hicho kiwe cha kusisitiza maadili, uaminifu, uadilifu na uzalendo”.
Aidha, Prof. Mwandosya aliongeza kuwa Bodi ya NBAA na Watanzania wana wajibu wa kujenga fikra ya kizalendo kwa taifa lao na kujiamini katika masuala ya hesabu za fedha ili waweze kufikia viwango vya kimataifa kwa kuweka misingi imara kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ambapo mataifa mengine wavutiwe kuja kujifunza hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa taarifa ya Bodi hiyo kwa mgeni rasmi wakati wa maafali hayo alisema kuwa kituo hicho kimefanikiwa kinatoa mchango mkubwa nchi katika kukuza fani ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma. 
Katika mahafali hayo, idadi ya wahitimu imeongezeka mwaka huu na kufikia 972 waliopata CPA na wahitimu 87 kwa ngazi ya cheti cha utunzaji wa hesabu tofauti na hali ilivyokuwa mwaka jana 2014 ambapo kulikuwa na jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
Wakati huo huo, mmoja wa wahitimu hao Imelda Mzatulla alisema kuwa kiapo walichoapa kinawahamasisha kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa kanuni za maadili ya kiuhasibu na ukaguzi wa hesabu, kwa uaminifu, uadilifu na utaalamu kwa kuzingatia matarajio ya Serikali, muajiri, jamii na taifa kwa ujumla.
Kiapo hicho walichoapa wahitimu hao, pia kinawahimiza kuwa waendelee kushirikiana na kituo hicho cha NBAA kwa kuzingatia miongozo yote ya taaluma yao inayotolewa na Bodi hiyo nchini.

No comments: