Saturday, October 03, 2015

SKYLIGHT BAND KUSINDIKIZA TAMASHA LA FAHARI YA MWAFRIKA NDANI YA KIOTA CHA ESCAPE ONE LEO JUMAMOSI OCTOBA 3, 2015

 Mmiliki wa Skylight Band Dk Sebastian Ndege(Jembe ni Jembe) akicheza moja ya nyimbo ya bendi Skylight. Njoo leo Jumamosi kwenye Show ya Fahari ya Mwafrika itakayofanyika kwenye kiwanja cha Escape One ambapo Skylight Band ikisindikizwa na Msanii machachari Barnaba Classic watadondosha moja ya show kali usisubirie kusimuliwa njoo wewe na yule.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa Skylight band waiimba na kucheza mbele ya mashabiki wao ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni.
Sam Mapenzi pamoja akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki  wa bendi hiyo (hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One Mikocheni.
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku wakiendelea kuzirudi nyimbo kali za Bendi hiyo.
Mashabiki wa Bendi ya Skylight wakiendelea kukata mauno kutokana na muziki mkali wa bendi hiyo jumapili iliyopita.
Ule muda sasa ulifika wa kusugua maana ilikuwa ni noma sana
Bendi haiwezi kuwepo bila kuwa na hawa jamaa wakali wanaosababisha Bendi ya Skylight kupaa.

No comments: