Thursday, October 01, 2015

RAIS KIKWETE KUZINDUA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU DAR ES SALAAM

unnamedcRais Kikwete anatarajia kuzindua Kituo Kituo cha Michezo cha Kisasa cha Jakaya M. Kikwete Youth Park (JMK Park), Kidongo Chekundu, Dar es Salaam, kituo cha kwanza cha aina yake nchini chenye kulenga miongoni mwa mambo mengi kuanza kulea wanamichezo tokea wakiwa wadogo.
Hayo yalijitokeza  wakati wa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion Power, Bwana Paul Hinks(pichani) kwenye Hoteli ya JW Marriot Essex House, mjini New York, Marekani ambako Rais alikuwa anafanya ziara rasmi ya kikazi. Rais Kikwete alikiwekea Kituo hicho jiwe la msingi mwaka jana.
unnamedv
Katika mkutano huo, uliofanyika jana, Jumanne, Septemba 29, 2015, Bwana Hinks alimweleza Rais Kikwete kuwa ujenzi wa Kituo hicho sasa umekamilika tayari kwa uzinduzi na hivyo kuongeza thamani kubwa kwenye eneo ambalo miaka ya nyuma lilikuwa gereji ya kutengenezea magari.
J
Kituo hicho cha JMK Park kimegharimu kiasi cha dola za Marekani milioni mbili na ni matokeo ya ushirikiano ya Kampuni ya Symbion Power ya Marekani, Klabu ya Soka la Ligi Kuu ya Uingereza ya Sunderland AFC na Taasisi ya Grasshopper Soccer.
(Picha na Freddy Maro).

No comments:

WANANCHI 216 WAKABIDHIWA HATI MILIKI WILAYANI MASWA

Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Simiyu, leo imeendesha zoezi la kugawa jumla ya hati miliki 216 kwa wananchi wa Wilaya ya Maswa....