Thursday, November 05, 2015

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YASAINI MKATABA WA JUMLA YA EURO MILIONI 158.5 NA SERIKALI YA UJERUMANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke (kushoto) wakati wa maandalizi ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
2
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke mara baada ya kusainiwa leo jijini Dar es salaam.
3
Ujumbe ulioshuhudia utiaji saini utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Wa pili kutoka mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile, kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer, Afisa Msimamizi wa Fedha Wizara ya Fedha Bw. Abdallah Lyangu, Mchumi kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Jan-Dieter Gosink na kushoto kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ni Mchumi Wizara ya Fedha Bw. Melckzedek Mbise kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliyofanyika Wizara ya Fedha.
4
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Ujerumani mara baada ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer pamoja na Mchumi ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw.Jan-Dieter Gosink.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya Euro milioni 158.5 na Serikali ya  Ujerumani wenye lengo la kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelie aliposaini mkataba huo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke leo jijini Dar es salaam.
Dkt. Likwelile alisema kuwa lengo kuu la fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Afya, Mazingira, Nishati, Maji na kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke alisema kuwa  nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa nchi hizo zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umekuwa na manufaa na tija kwa wananchi baina ya nchi hizo mbili.
Imetolewa na
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
04/11/2015

No comments: