Monday, August 17, 2015

SIMBACHAWENE AKABIDHI NYARAKA ZA UFADHILI KWA WATANZANIA 22 KUSOMA MAFUTA, GESI CHINA

x1x2
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (Kulia) akizungumza na  waandishi wa habari, baadhi ya Watumishi wa Wizara na wanafunzi  waliopata ufadhili wa  masomo katika ngazi za  Shahada za Uzamivu (Phd) na  Uzamili (Masters), katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.
x3
Baadhi ya wanafunzi 22 waliopata nafasi za masomo ya shahada za Uzamili na Shahada ya Uzamivu wakimsikiliza kwa kwa makini Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
x4
Waziri akiwakabidhi nyaraka za kusafiria na zenye maelezo baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masoma katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.Katikakati ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile.
x5x6
……………………………………………………………………..
Na Clinton Ndyetabula, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, amewakabidhi Nyaraka za  Ufadhili na kuwaaga wanafunzi 22 wa Kitanzania wanaokwenda  masomoni nchini China,  kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada za Uzamivu (Phd) na  Uzamili (Masters).
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Nyaraka hizo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es Salaam, leo, Simbachawene amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii ili hatimaye waweze  kusaidia Taifa katika kuendeleza sekta ndogo ya gesi ikiwemo kuanzisha vyanzo mbadala vya nishati ya umeme , kuongeza usimamizi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo, na kusaidia katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
“Kama mnavyoelewa Wizara yetu ni miongoni mwa Wizara zilizo katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika sekta ya Nishati. Mpango huu unategemea kutoa matokeo makubwa ya haraka, na hili kutekeleza ipasavyo tunahitaji  wataalamu wazalendo waliobobea katika fani za ,mafuta na gesi asilia” alisema Simbachawene.
“Ni matumaini yangu kuwa mtatumia vizuri fursa mliyopata, mtajifunza kwa bidii na  kuiwakilisha nchi yetu vizuri na  kuleta  teknolojia  zitakazosaidia kupata ufumbuzi au mapendekezo  ya namna ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta hii”alieleza Simbachawene
Aidha, Waziri alitumia nafasi hiyo kuishukuru  Serikali ya Jamuhuri ya Watu  wa China kwa kuwawezesha Watanzania  kusoma masuala ya mafuta na gesi  tangu mwaka 2013 na kuongeza kuwa , serikali hiyo  imeahidi kuendelea kutoa ufadhili  kwa watanzania katika ngazi za Shahada ya Uzamivu na Uzamili hadi  ifikapo mwaka 2019.
Aidha, Simbachawene ameeleza kuwa, Wizara ilipokea jumla ya maombi 187 na kati yao, waombaji 33 waliokidhi vigezo walichunjwa na Serikali ya Watu wa China na kupatikana washindi 22.

No comments: