Wednesday, August 26, 2015

WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA WATEMBELEA ESTONIA

x1
Wandishi wa habari kutoka Tanzania katika picha na mwakilishi wa kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya Nortal muda mfupi baada ya kumtembelea kampani hiyo jijini Tallinn Estonia
x2
Meya wa mji wa Haapsalu katika picha ya pamoja na baadhi ya wandishi wa habari wa Tanzania baada ya nazungumza na wandishi hao.
………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza
Wandishi wa habari sita kutoka vyombo vya habari kutoka Tanzania wako ziarani chini Estonia kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo.
Lengo la ziara hiyo ni kutoa fursa kwa wandishi wa habari wa Tanzania kujifunza na kujionea shughuli mbali mbali katika sekta za teknolojia ya mawasiliano , elimu, utalii, afya n.k. ili kuandikia habari hizo n chini Tanzania.
Katika siku mbili za mwanzo za ziara hiyo ya siku tano,  wandishi hao kutoka Tanzania 
tayari wametembelea sehemu kadhaa ikiwa ni pamoja na kampuni kubwa inayoongoza katika teknolojia ya mawasiliano chini Estonia iitwayo Nortal, kituo cha tiba maalumu ya matope na chumvi kilichopo katika mji wa Haapsalu na kuzungumza na Meya wa mji huo Staili Meya Maret Sukles.
Katika ziara hiyo inayoratibiwa a na chuo kikuu cha Tullinn shule kuu ya Media and filming ya Balticts, wandishi hao wamefuata na afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Sweden Bw. Jacob Msekwa. 
Post a Comment