Monday, August 31, 2015

PSPF WATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI YA MADEREVA WA BODABODA WA KIPUNGUNI DAR ES SALAAM

 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akitoa somo kwa madereva bodaboda kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari(PSS) waliofika katika mchezo wa fainali katika uwanja wa Kipunguni B
Mmoja wa Madereva Bodaboda akiendelea kupewa faida za mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto)
Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijisajili kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) kwa ajili ya kuendelea kupata huduma zilizobora na  zenye uhakika kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy 
Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijiunga kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) ambapo kila mtu anaweza kujiwekea akiba kupitia kwenye mfuko huo wa hiari wakati wa mchezo wa fainali.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akiwasajili madereva wa Bodaboda kwenye mfiko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS)  wakati wa mchezo wa fainali wa Madereva bodaboda ambapo G Unity aliibuka mshindi kwa kumchapa Sukuma Land bao 5-2
Vijana waliofika katika mchezo wa fainali wakisoma vipeperushi vya mfuko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ambapo mfuko huo ulidhamini ligi hiyo iliyoendeshwa kwa wiki nzima Continue reading →
Post a Comment