Friday, August 21, 2015

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA SHULE YA SEKONDARI DODOMA


 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,  Rehema Mkamba akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.
 
 Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Dodoma, Marco Masala akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi  vilivyotolewa na LAPF.
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Rehema Mkamba akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF
      Baadhi ya Wanafunzi wa Dodoma Sekondari waliohudhuria hafla hiyo.
 Mwanafunzi wa kidato cha sita Sabina John akitoa neon la shukurani kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma. 

Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo hii unakabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shillingi millioni mbili kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uzio,baada ya kupokea ombi la kuchangia ujenzi huo.

LAPF inaamini kuwa msaada huu utasaidia kuchangia gharama na hatimaye kufikia lengo la kukamilisha ujenzi huo na kuhakikisha usalama wa wanafunzi. Msaada huu utawanufaisha si  tu Wanafunzi na  Walimu wa Shule ya Sekondari Dodoma bali pia wadau wengine mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia viwanja vya Shule hii kwa michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na watumishi wa LAPF.

LAPF imekua ikitoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa wadau muhimu kama Shule za Msingi na Sekondari,Vituo vya Afya, Vituo vya Watoto yatima , kuchangia michezo nk.
LAPF ni Mfuko wa Pensheni ambao  pamoja na majukumu mengine, jukumu lake kuu ni kutoa mafao ya Pensheni kwa wanachama wake. Mafao yanayotolewa na LAPF ni pamoja na;
·         Pensheni ya Uzeeni.
·         Pensheni ya Ulemavu.
·         Pensheni ya Urithi.
·         Fao la Uzazi.
·         Mikopo ya kujikimu.
·         Mikopo ya elimu .
·         Mikopo ya nyumba.
·         Mikopo kwa wanachama wa kupitia Saccos.
·         Mikopo kwa Wastaafu.na
·         Msaada wa mazishi.
Kwa sasa Mfuko wa pensheni wa LAPF unaandikisha wanachama kutoka sekta zote kama vile Waalimu, Watumishi wa Afya, Wajasiliamali nk.

MAISHA POPOTE NA LAPF

No comments: