Friday, August 28, 2015

MWENYEKITI WA TAASISI YA SEKTA BINAFSI NCHINI (TPSF) DK REGINALD MENGI AFUNGUA MAONYESHO YA MAFUTA NA GESI MLIMANI CITY


Maonesho ya ya bidhaa za viwandani yatakuwa na manufaa zaidi kwa Tanzania iwapo makampuni Makubwa ya kutoka nje ya nchi yatazalisha bidhaa hizo hapa hapa nchini.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini - TPSF Dr. Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua maonesho ya siku tatu ya Mafuta na Gesi yaliyoratibiwa na Kampuni ya EXPOGROUP, kwa kushirikiana na TPSF.
Amesema Maonesho ya aina hiyo ni mazuri kwa kuwa yanatambulisha bidhaa na teknolojia mpya sokoni. Hata hivyo amesema Watanzania hawapaswi kuwa watazamaji tu, bali watumie mwanya huo kuyashawishi makampuni hayo kutengeneza bidhaa zao hapa hapa nchini.
Baada ya uzinduzi wa maonesho hayo, na machapisho yake, Dr Mengi, aliyefuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye, walitembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho kujionea bidhaa mbalimbali, na alipofika banda la kampuni ya Tanzania ya  Simba Traillers, Mkurugenzi wake Hussein Dewji amesema kampuni yake inatengeneza matela ya magari makubwa hapahapa nchini.
Mapema Meneja wa Maonesho hayo yanayoshirikisha makampuni 80 kutoka nchi 24 duniani Bw. Neville Trindade na Afisa Uendeshaji wa EXPOGROUP BW. Pius Gechamet wamesema lengo la maonyesho hayo ni kuvutia uwekezaji na wamewataka Watanzania kuchangamkia maonyesho hayo yatakayodumu kwa siku tatu.
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Juliana Mataba akimfafanulia jambo Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini - TPSF Dr. Reginald Mengi  wakati mgeni huyo alipotembelea banda la maonyesho la Shirika. Kulia anayefuatilia mazungumzo hayo ni Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai.
Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizungumza katika maonyesho hayo ambayo NHC ni mshiriki.
Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizindua kijarida katika maonyesho hayo ambayo NHC ni mshiriki.
 Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizungumza katika maonyesho hayo ambayo NHC ni mshiriki.
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Juliana Mataba akimfafanulia jambo Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald wakati mgeni huyo alipotembelea banda la maonyesho la Shirika. Kulia anayefuatilia mazungumzo hayo ni Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai.

No comments: