Friday, August 21, 2015

RAIS KIKWETE APOKEA HATI YA UTAMBLISHO WA BALOZI WA DENMARK NCHINI

kj1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea hati ya utambulisho ya Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kujitambulisha.
kj2
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen akisaini kitabu cha wageni wakati alipokuwa anaenda kukabidhi hati ya utambulisho na kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
kj3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
kj6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kushoto) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
kj7
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalimu (wa pili kushoto) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
kj8
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) akiwa amesimama wakati nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark zikiimbwa leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
kj9
Bendi ya Jeshi la Polisi nchini ikipiga nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark wakati Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) alipokuwa anakwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

No comments: