Saturday, August 22, 2015

SUMAYE AITOSA CCM, AJIUNGA UKAWA


Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akiongea na wanahabari.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, leo  amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Sumaye amejiunga rasmi na Ukawa wakati wa mkutano wa wanahabari na viongozi wa Umoja huo,  mkutano uliofanyika mchana wa leo katika ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar.
Aidha Sumaye hakusema ni chama gani amejiunga nacho, licha ya kubainisha lengo lake kuu la kuondoka CCM ni kwenda kuimarisha Ukawa na kuongeza nguvu kwenye vyama vya upinzani hasa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

No comments:

RAIS SAMIA AMKARIBISHA RAIS WA NAMIBIA KATIKA ZIARA YA KITAIFA, WAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA MAENDELEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Dkt....