Friday, August 21, 2015

JIONE PICHA VYAMA VYOTE VILIVYORUDISHA FOM NEC LEO




Mgombea Urais kupitia ADC, Chief Lutasola Yemba amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia Chama cha UMMA, Hashim Rungwe amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia UPDP Fahmi Nassoro Dovutwa amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Bi. Anna Elisha Mghwira amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wagombea wengine kwa ufupi ni;

CHAUMA Rungwe amethibitishwa na Jaji tayari

John Dustan Chipaka kaingia ofisi za NEC na yeye,

chama cha NRA Janken Kasambala na mgombea mwenza Samai Abdulla wamewasili tayari wamethibitishwa na jaji

CCK wameshindwa kukidhi vigezo na masharti ya Tume, wenyewe kupitia kwa DKt. Malisa wamesema "Tumefungua shitaka mahakamani hivyo nategemea tume isitishe kwanza mchakato"

Chipaka wa TADEA nae akataliwa na tume kwa kuwa hajakidhi vigezo


Mch. Mtikila wa DP kakataliwa kwani hakukidhi vigezo. Alienda kuapa bila mgombea mwenza hivyo hakuapishwa.NEC yasema Ikifika saa kumi watafunga zoezi hilo, Mch. MTIKILA amerejea eneo la NEC na kuambiwa hajakidhi Vigezo, Yeye kasema Kukosa kugombea Urais hakutanizua kwenda Mbinguni.

Jumla ya Vyama nane na Wagombea wao, wamefanikiwa kurudisha fomu na wameidhinishwa na Tume ya Uchaguzi na wanaweza kuanza kampeni muda wowote kwa kuzingatia maadili na masharti ya tume ya kuendesha zoezi la kampeni.

Vyama vilivyo fanikiwa kuthibishwa na kukidhi vigezo ni;

UPDP

CHADEMA

CCM

TLP

ADC

ACT

CHAUMA

NRA

Vyama ambavyo havikukidhi vigezo ni;

TADEA

CCK

AFP- Mgombea hakuonekana kabisa wala fomu hajikurudishwa.

No comments: