Wednesday, August 26, 2015

LAWRENCE MASHA AACHIWA HURU

 Masha aliyevaa tisheti jeusi suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu akifurahia jambo na wenzake muda mfupi baada ya kupata dhamana

Kwa ufupi
Masha aliachiwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuithibitishia mahakama kuwa nyaka hizo ni halali.
--
Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam.
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Masha alifikishwa mahakamani hapo jana nyakati za saa 6:49 mchana na kuhifadhiwa mahabusu na ilipofika saa 9:31 alasiri alipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu, Waliarwande Lema kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Masha aliachiwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuithibitishia mahakama kuwa nyaka hizo ni halali.

Kufanyika kwa uthibisho huo wa nyaraka za wadhamini ndio uliopelekea juzi Masha kupelekwa mahabusu katika gereza la Segerea.

Baada ya kumaliza kukamilisha taratibu hizo za dhamana ilipofika saa 9:46 alasiri Masha, mkewe, mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo, Peter kibatala na Albart Msando pamoja na ndugu zao wengine waliondoka mahakamani hapo kwenda nyumbani.

Awali Agosti 25, 2015 Masha alipandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha ya matusi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi.

Masha aliyekuwa amevaa tisheti jeusi, suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu na viatu aina Sendo anadaiwa kuwa Agosti 24,2015  katika kituo cha polisi cha Osterbay alitoa lugha ya matusi kwa maofisa wa jeshi la polisi.

No comments: