NSSF YASHIRIKI KWENYE MKUTANO WA MWAKA WA WADAU WA KOROSHO MKOANI LINDI LEO

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki kwenye mkutano wa Wadau wa Korosho unaofanyika kwenye Hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi,mkutano huo utakaofanyika kwa Siku mbili mfululizo utahusisha wadau wa Korosho kutoka Tanzania nzima.

Katika Mkutano huo ambao NSSF imepata nafasi ya kutoa  mada imewahimiza wadau hao waweze kujiunga na NSSF ili waweze kupata mafao bora yatolewayo na mfuko huo, Mafao hayo yakiwemo Matibabu bure, Kuumia Kazi, Uzazi kwa Kina mama , Mikopo kwa wanachama na Mengineyo.

Akiongea katika Mkutano huo Meneja wa NSSF Mkoa wa Mtwara , Stanley Milanzi amewaambia wadau huo kupitia Mpango wa NSSF Wakulima Scheme wakulima wa Mkoa wa Mtwara wamepata karibia Shilingi bilioni mbili kama mikopo kutoka NSSF.
 
Meneja Kiongozi wa Masoko na Uhusiano  wa NSSF, Eunice Chiume(wa tatu Kushoto)  akiwa na Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi, Jumbe Dona (wa pili Kushoto), Afisa  Matekelezo Kuruthum Yusufu ( Wa kwanza Kushoto), Afisa Mwandamizi wa Uhusiano Salim Kimaro (wa tatu Kulia), Afisa Uendeshaji Muandamizi Abasi Cothema (wa pili Kulia) na Afisa Mafao wa Mkoa wa Lindi Paschal Mushi (Wa kwanza Kulia) kwenye mkutano wa Wadau wa Korosho unaofanyika leo katika hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi.
Maofisa wa NSSF wakiwasaidia wadau wa Korosho kujaza fomu za uanachama ili waweze kujiadikisha kujiunga na NSSF.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.

Meneja Wa NSSF Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi  akiwaelekeza wadau wa Korosho jinsi ya kujaza fomu za NSSF ili waweze kujiandikisha na NSSF.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.

Comments