Thursday, August 27, 2015

RUVU JKT ILIVYOWAKILISHA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KUONYESHA MAFANIKIO YA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAJESHI NCHINI

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa kuiwakilisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha mafanikio ya majeshi nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa mgeni rasmi katika ziara hiyo ya siku moja ya waandishi wa habari kutembelea kikosi hicho. Kingu alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto), akiwaelekeza wanahabari wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya mazoezi ya gwaride la kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi ujao.

No comments: