Friday, August 21, 2015

LOWASSA AREJESHA FOMU NEC LEO NA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA HALALI WA CHADEMA


 Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachoungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea Urais katika uchaguzi utakao fanyika Oktoba 25, 2015. Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ndie aliyepokea fomu hizo na kutangaza rasmi kumteua Edward Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Haji Duni kuwania nafasi hizo kupitia vyama vyao.
 Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akizungumza.
 Mwenyekiti wa Tume akisaini fomu hizo...
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akizungumza.
 Lowassa akitoka ofisi za NEC huku akisindikizwa na viongozi wa UKAWA.
Lowassa akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu. SOURCE:FATHER KIDEVU.

No comments: