Monday, August 24, 2015

Zaidi ya vijana 1000 wapata mafunzo bora ya Kilimo

Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture” iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Kushoto ni Doris Chaula na Faraja Alex ambao ni washiriki wa semina hiyo.
Mkulima wa Mkoa wa Arusha Faraja Alex(kulia)aliyeshiriki katika semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture”akisalimiana na Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(katikati)wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Anayeshuhudia kushoto ni mshiriki wa semina hiyo Doris Chaula.
MWenyekiti wa Taasisi ya AMSHA,Biubwa Ibrahimu(katikati)akimsikiliza jambo maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(kushoto) wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture” iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Kulia ni mshiriki wa semina hiyo Faraja Alex.
Washiriki wa semina ya Vijana iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture” Bi. Doris Chaula na Faraja Alex(kulia)wakimsikiliza jambo Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(katikati)wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu.

Zaidi ya vijana 1000 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walihudhuria katika semina ya kupambana na wimbi kubwa  la ajira.Semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na kuhuthuriwa na zaidi vijana 1000 ilikuwa na kauli mbiu isemayo “Kilimo Biashara Ndio Mpango Mzima”-Agribusiness is the real deal na  vijana wengi walitoa mawazo yao na kuelezwa fursa  mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya kilimo na jinsi gani zinaweza kuwakwamua kiuchumi na kujiajiri wao wenyewe baadhi ya sekta hizo zikiwa za ufugaji,upandaji wa miti,kilimo cha kisasa na jinsi ya kusindika mazao na kuyapeleka kwenye masoko.

Akiongea kwa niaba ya washiriki wenzake Bw.Jason Kato ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu alisema kuwa semina kama hizi ni muhimu kuwafikia wananchi wengi na kuwafungua akili  kujua kuwa kilimo ndio silaha pekee ya kuondoa tatizo la ajira nchini hususani kwa vijana badala ya kufikiria kuwa kilimo sio kazi au ni kazi ya watu walioshindwa maisha.

Naye Meneja wa huduma ya Kilimo Klabu inayotolewa na Vodacom Tanzania, Bw.Frank Madembwe alibainisha kwamba huduma ya matumizi ya teknolojia ya simu ya mkononi inayotolewa na kampuni yake imeelezwa kuwa imeanza kuonyesha mafanikio makubwa na ni silaha ambayo itaondoa umaskini nchini kupitia  sekta ya kilimo iwapo itatumika ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Meneja huyo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini na kushirikisha  mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali yanayoshughulika na kilimo na kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Bw.Medembwe alisema kuwa kutokana na matumizi ya simu za mkononi kuongezeka nchini,Vodacom ikiwa ni kampuni inayoongoza kuwa na mtandao mkubwa nchini iliona umuhimu  wa kubuni huduma za kurahisisha maisha ya watanzania ambao wengi ni wakulima wanaoishi vijijini na ndio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikaibuka na huduma ya kilimo Klub.

Alisema ndani ya Kilimo Klub kuna huduma mbalimbali zinazopatikana ambazo zimerahisisha maisha ya wakulima ambazo ni M-Pesa,huduma ambayo imeleta ukombozi kwa kurahisisha utumaji fedha na upokeaji fedha bila kusahau kufanya mihamala mbalimbali ya Malipo pia ipo huduma ya M-Pawa inayowezesha mtumiaji wake kujiwekea akiba kupitia simu yake ya mkononi na Kujipatia mkopo wenye masharti nafuu .

Aidha madembwe alisema ipo huduma ya M-Kopa inayowawezesha wakulima hususani sehemu ambazo hazijafikiwa umeme kupata nishati hiyo  kwa kupatiwa vifaa vya umeme unaotumia jua kwa mkopo na unafuu wa bei pia kuna huduma ya Sokoni inayowawezesha wakulima kupata taarifa za bei za mazao.

“Kupitia Kilimo Klub tunaamini kuwa mabadiliko makubwa yatatokea katika sekta ya kilimo kuanzia kwa wakulima wenye mpaka kwa wanunuzi wa mazao ya wakulima na hii inadhihirisha kuwa teknolojia ikitumika ipasavyo inaweza kuleta  mabadiliko makubwa kama ambavyo tumeanza kushuhudia”.Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Taasisi ya MKURABITA ambaye alikuwa mgeni rasmi Bi.Serapia Mgembe alisifu jitidaza zinazofanywa na taasisi mbalimbali hususani zinazoshughulika na kuinua wakulima nchini kwa kuwa bado kuna fursa nyingi kwenye sekta hiyo na aliwataka vijana kuchangamkia kilimo biashara ili kuboresha maisha yao.

Taasisi nyingine ambazo zilizowaoa vijana kuhusu kilimo zilishoshiriki semina hiyo ni Agri pro Focus,ANSAF,AMSHA, na Tanzania Graduates Farmers Association,pia kulikuwepo na maonyesho ya mazao ya kilimo kutoka vikundi vya  kilimo na usindikaji wa mazao ambapo pia washiriki waliweza kupata maelezo jinsi huduma ya M-Kopa inavyotolewa kupitia mitandao wa Vodacom na vituo vya mawakala wake.
Post a Comment