Monday, August 24, 2015

LOWASSA AZUNGUKA NA DALADALA HADI GONGO LA MBOTO KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI


Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi, UKAWA, Edward Lowassa leo ametembelea maeneo ya Gongo la Mboto na kuzungumza na wananchi kadhaa akitumia usafiri wa daladala.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar
es salaam leo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi.

Post a Comment