KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘CHAGUA TIGO PESA, INALIPA

 Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya ya Chagua Tigo Pesa, Inalipa. Kulia ni Meneja  Bidhaa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja  Bidhaa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya tigo Tanzania imezindua Kampeni iitwayo”chagua tigo pesa,inalipa”ikiwa na lengo na la kuongeza upatikanaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi kwa wateja.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Ruan Swanepoel alisema huduma hiyo ikiwa na muonekano mpya na sura kwa wateja wake wanaotumia huduma ya tigo pesa Tanzania nzima.
Alisema kuwa kwasasa mtandao wa tigo umeenea kwa wingi hapa nchini na unatumiwa na asilimia 90 ya wananchi wote wanaomiliki simu za mkononi.
Alisema kuwa mtandao wa tigo unakikisha inatoa huduma stahiki kwa wateja wakena kuhakikisha huduma ya tigo pesa inazidi kuwa na huduma pendwa kwa sababuinapatikana kirahisi na makini.
Alisema kuwa huduma hii inalipa kwa wateja wake na kukopa fedha hasa kwa wale wenye kipato kidogo na wasio na huduma za kibenki.
Alifafanua kuwa wateja wa tigo pesa watanufaika na kampeni hii kwa kuypata vifurushi vya bure kila wannunuapo bidhaa na kulipia kwa tigo pesa kutoka kwa wauzaji waliosajiliwa.
Pia aliongeza na kusema kuwa wateja watapata riba kila baada ya miezi mitatu kulingana na kiasi cha fedha ya kifurushi ambacho mteja atamnunulia mtu mwingine kwa tigo pesa.

Comments