Meneja Mafunzo ya Biashara wa Airtel Tanzania, Ayubu Kalufya akitoa
elimu kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Meneja Mauzo wa Airtel Tanzania Kanda ya Ilala, James Moilo akitoa
elimu kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo
kwa mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Wakala wa Airtel Money Tabata, Sabas Ngwira akiuliza swali kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Wakala wa Airtel Money Ukonga, Grace Kimaro akiuliza swali kuhusu
huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa mawakala
wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Sehemu ya Mawakala wa Airtel Money mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, iliyofanyika
jijini jana.
KAMPUNI ya Simu za Mkoni ya Airtel imetoa semina kwa Mawakala wa Airtel Money zaidi ya 400 kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali za ujasiriamali huku wakinufaika kupitia huduma ya mikopo kwa wateja maarufu kama Timiza Mkopo kwa Wakala.
Kupitia semina hiyo mawakala wa Kampuni hiyo wataweza kuona fursa
mbalimbali za kibiashara na kutumia mikopo hiyo isiyo na dhamana
watakayopata kutoka Airtel kukuza biashara zao na kuongeza mitaji.
Akizungumza wakati wa Semina hiyo Meneja Mauzo wa Airtel Money Moses
Alphonce alisema kupitia mafunzo hayo mawakala wataweza kuongezea
faida zaidi na hatimaye kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini.
“Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitumia mikopo wanayopata kwa ajili ya matumizi ya kawaida, kupitia semina hii, mbali ya kuwaunganisha mawakala wetu wa Jijini pia watafahamu mbinu bora za kutenganisha fedha za mtaji na binafsi,” alisema Alphonce.
Kuhusiana na namna mawakala hao wanavyoweza kuchangia kukuza uchumiAlphonce alisema, fedha watakazokopa zinaweza kuanzisha biashara nyingine itakayoingiza kipato na kutoa ajira kwa ndugu na jamaa wanaowazunguka.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Biashara wa Financial sector Deepening
Trust(FSDT) Innocent Ephram ambaye alikuwa Mwezeshaji wa semina hiyo
amesema wajasiriamali wengi wameshindwa kukuza biashara zao baada ya
kuchanganya matumizi ya biashara na ya kwao binafsi.
“Kupitia warsha hii wajasiriamali watapata fursa ya kufahamu athari za
kuchanganya matumizi ya biashara na maisha ya kila siku, jambo ambalo
linachangia hasara na kufa kwa mtaji,” alisema Mtaalam huyo kutoka FSDT.
Baadhi ya mawakala hao kutoka Manispaa zote tatu za Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Salama Sinani,Gorich Mlaki na Sabas Ngwillah walisema mafunzo hayo sasa yamewapa mwanga wa kuifanya kazi hiyo kama ajira na tofauti na awali ambapo waliiona kazi ya uwakala kama jambo la ziada tu.
“Nilikuwa naona kazi ya uwakala kama kazi ya ziada, sasa nitaweza kuchukua mkopo kupitia Timiza Mkopo kwa Wakala nitaanzisha biashara nyingine itakayonikomboa kuondokana na umaskini,” alisema Gorich Mlaki anayefanyia kazi zake Hospitali ya taifa Muhimbili jijini.
Agosti 18 mwaka huu Airtel ilizindua mkopo huo utakaoanzia Shilingi 50,000
hadi 500,000 utakawanufaisha zaidi ya mawaka 20,000 wa Airtel Money.
utaendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na Afb Tanzania.
Comments