Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
wa timu ya Harmburg Queens Jamila Kassim baada ya kuwa mabingwa katika
michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Ilala. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya Evergreen Linda Shilla baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Temeke. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
wa timu ya Wakati Ujao FC Alphonce Peter baada ya kuwa mabingwa katika
michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
wa timu ya Sylivia Mwacha baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka
wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
wa timu ya Sylivia Mwacha baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka
wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Wachezaji wa timu ya Mchanganyiko FC wakishangilia baada ya kuwa
mabingwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe
ilifanyika jana katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini
Dar-es-Salaam.
MICHUANO ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Aitel Rising
Stars kwa mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke jana ilifungwa
rasmi katika uwanja wa Karume ambapo mabingwa wa mikoa husika
walikabidhiwa zawadi zao.
Kwa upande wa wasichana, Hamburg Queens walifanikiwa kutawazwa
mabingwa wa mkoa wa Ilala huku Bombom wakitwaa taji la ubingwa wa mkoa huo kwa upande wa wavulana.
Katika mkoa wa Temeke upande wa wasichana, timu ya Evergreen ndio
walitangazwa mabingwa na Wakati Ujao ndio walioibuka wababe kwa upande wa wavulana katika mkoa huo.
Kwa mkoa wa Kinondoni, timu ya wasichana ya Mburahati Queens
walifanikiwa kuwa mabingwa wakati Mchanganyiko FC wakitangazwa
mabingwa kwa upande wa wavulana.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando, alitoa shukrani zake za
dhati kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na vyama
vya mikoa kwa ushirikiano wao ambao unawapa nguvu ya kuendelea
kudhamini programu hiyo ya soka kwa vijana.
“Mwaka huu tumeshuhudia uboreshaji mkubwa zaidi wa mashindano haya
baada ya ujio wa timu za wasichana ambao wameongeza msisimko wa
michuano hii. Pia naamini tutapata wavijana wenye vipaji ambao
watasaidia kutangaza taifa letu hapo baadaye katika ngazi za
kimataifa”, alisema Mmbando.
“Shukrani zangu nazipeleke pia kwa Makatibu wa mikoa shiriki kwa
kufanikisha kupata vijana bora na wenye weledi ambao ni nuru ya taifa
letu kwa siku za usoni”, aliongeza.
Kwa upande wake mgeni rasmi, Boniface Wambura ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, alisema anaipongeza Airtel kwa mchango wao hapa nchini wa kuvumbua vipaji vya vijana ambao ni manufaa kwa taifa kwa
siku za baadaye.
“Nimefarijika kuona vijana wakijituma na kucheza kwa ari kubwa licha
ya umri wao mdogo, jambo ambalo litawafikisha mbali katika maisha yao
ya soka, kitu cha msingi ni kuhakikisha hamkati tama ili kuweza
kufikia malengo” alisema Wambura.
“Sisi TFF, tutahakikisha michuamo yote inayohushisha vijana
inaendeshwa kwa weledi wa hali ya juu ili kupata vijana bora
watakaoweza kulisaidia taifa letu kuanzia timu za vijana mpaka za
wakubwa hapo baadaye”, Wambura aliongeza.
Wakati huo huo mikoa hiyo mitatu ya kisoka jana imeanza kutoana josha
katika mashindano ya Airtel Rising Stars yenye lengo la kupata
mabingwa wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya Chama cha Mpira wa soka
mkoani wa Dar es Salaam (DRFA).
Katika michezo miwili iliyochezwa jana timu ya Ilala Girls iliibuka na
ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Temeke Girls wakati timu ya
wavulana, Ilala Boys walipepetana na Temeke Boys ambapo Ilala Boys
waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha
mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha
inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa
kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11
hadi 21.
Comments