Monday, August 17, 2015

DJ WA NIGERIA KUFANYA ONYESHO NA KUTOA MSAADA KWAJAMII JIJINI DAR ES SALAAM

 Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence Ifeoluwa maarufu kama DJ Cuppy akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway jijini Dar  es Salaam.
Baadhi ya wa habari wakiwa na Dj Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia Nigeria katika hoteli ya Silpway jijini Dar es salaam.
DJ Cuppy.

 MTENGENEZAJI wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence Ifeoluwa
 maarufu kama DJ Cuppy amewasili jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika yenye jina la 'Cuppytakes Africa'. 

Wakati akiwa jijini hapa Dj huyu ambaye ni maarufu sana alitembelea kituo chaKigamboni Community Center kinachotoa elimu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 

Ziara yake ilihitimishwa na onyesho la muziki lililofanyika katika hoteli ya Slipway,tarehe 16 Agosti,Ziara yake hii kabambe ya mwezi mzima ilianza Agosti 1 jijini Lagos, Nigeria ikifuatiwa naSenegal, Ghana na Kenya. 

Tanzania ni nchi ya tano katika ziara yake na hapo DJ Cuppy atatembelea nchi za Rwanda, Uganda na Afrika Kusini.“Nilikuwa na ndoto ya kutembelea Afrika, lengo kuu likiwa ni kujionea utamaduni wake, ndotohii sasa imetimia," alielezea katika mkutano na waandishi wa habari mjini Lagos Julai 8 hukuakiongeza kwamba “nina furaha sana kuonja radha ya muziki tofauti na kupata uzoefu kutokanana ziara hii!" Alisema.

Pamoja na hayo, ziara hii inalenga kutoa msukumo katika jamii kwa kila nchi, DJ huyu mwenyekusherehesha ana shauku juu ya elimu ya viongozi wa baadaye wa Afrika. 

Kupitia msaadamkubwa wa asasi ya Dangote Foundation, anatembelea na kutoa msaada kwa shirika lisilo lakiserikali katika kila nchi atakayoitembelea. 
Hapa  Cuppy ametembelea kituo cha jamii cha Kigamboni kijulikanacho kama (KCC), Kituo hiki huwa kinashughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali na upatikanaji waelimu.

KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi, Ziara hii inayojulikana kwa jina la “Cuppy takes Africa” wamechagua kituo hiki kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipajina kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.

DJ Cuppy amefanya kazi katika safu ya tuzo yenye hadhi ya juu ikiwa ni pamoja na FinancialTimes Summit mwaka 2014 na kwenye tuzo za muziki za MTV Afrika. Yeye ni msomi kutokaChuo cha London King’s College na sasa anaendelea na masomo ya shahada ya uzamili katika


fani ya Sanaa na biashara ya muziki kwenye Chuo Kikuu cha New York. Cuppy pia ni balozi wautalii wa Nigeria.Ziara hii ya “Cuppy takes Africa”' inayojumuisha maonyesho, mashirikishano ya wasanii, fursaza vyombo vya habari na ushirikiano wa hisani umedhaminiwa na benki ya GT.

 Kuhusu DJ Cuppy:    
Cuppy ni DJ, producer wa muziki na mtunzi wa nyimbo.alizaliwa jijini Lagos mwaka 1992. Cuppy alianza kufanya uzalishaji wa muziki na baadayekuwa mchezesha muziki (DJ) akiwa na umri wa miaka 17.Cuppy mara nyingi amekuwa na bahati ya kuwa DJ kwenye umati wa watu wasomi wakimataifa; alitoa burudani mbele ya wanadiplomasia kwenye mkutano wa Financial Times Luxury mwaka 2014, ambao ulifanyika jijini Mexico City. Alikuwa pia DJ katika jarida la Tatlerna Christie Inc Arts Ball, ambao ulifanyika jijini London ikifuatiwa na matukio mengi yaushirika mjini Dubai. Kuchaguliawa kwa Cuppy kuwa Dj wakati wa tuzo za muziki za MTV Afrika mwaka 2014 mjini Durban, ilikuwa ni fahari kwa mashabiki wa Cuppy duniani kote.

 Mwaka jana mwezi Julai 2014, Cuppy ilitoa tepu yake iliyokuwa na mafanikio makubwailiyojulikana kwa jina la House Of Cuppy. Ikiwa na mkusanyiko wa radha ya muziki tofauti wawasanii wa kinigeria waliokuwa wanafanya vizuri kimuziki nchini Nigeria. House Of Cuppyilizinduliwa kwa mafanikio jijini London, Lagos na New York.Cuppy aliteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni na Utalii tarehe 17 Aprili 2014 kuwa Balozi wa utalii nchini Nigeria. Kwa sasa yeye ni nembo ya kuchochea kampeni ya kuitangaza Nigeria.
“Cuppy ni kijana mjasiriamali, na ni dhahiri anapaswa kuigwa.

No comments: