Wednesday, August 19, 2015

BUNGE LA VIJANA LAENDELEA BUNGENI DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi wake wa kuwajengea Uwezo Wabunge na Watumishi (LSP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa mara ya Pili mwaka huu limeratibu Bunge la Vijana kwa kushirikisha Wanafunzi zaidi ya 100 kutoka Taasisi za Elimu ya Juu hapa Nchi ambao ni viongozi katika Serikali zao. Bunge hilo ambalo limeanza Jumamosi tarehe 15 Julai, 2015 na linatarajiwa kumalizika tarehe 19 Julai 2015
A
Mbunge wa Bunge la Vijana Shughaib Abdi (CBE) akielezea baadhi ya mapungufu yaliyopo katika Muswada huo wakati wa Mjadala wa kujadili Muswada huo Bungeni
B
Wajumbe wa Bunge la Vijana wakishiriki Vikao vya Bunge hilo Mjini Dodoma
C
Waziri Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Alexandra Wasonga (ARDHI) akijibu Maswali ya papo kwa papo Bunge wakati wa Kipindi cha Masuali kwa Waziri Mkuu
D
Waziri kivuli wa Vijana kutoka Kambi Pinzani kwenye Bunge la Vijana Bi. Joyce Shirima akielezea baadhi ya Mapendekezo ambayo yanastahili kuingizwa kwenye Muswada wakati wa Majadiliano Bungeni
E
Daudi Maneno (MUST) nae akitoa dukuduku lake wakati wa Majadiliano Bungeni
F
Mwanasheria Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Gama Zulu Leonidas (SAUT) akiwasilisha Muswada wa Serikali wa Kuanzisha sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2015 Bungeni jana. 
G
Spika wa Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Baraka Thomas (UDSM) akiongoza vikao vya Bunge
JK
Bakari Ibrahim (MKWAWA) akiwasilisha Mchango wake kuhusu Muswada huo Bungeni

No comments: