Tuesday, December 01, 2015

PINDA ATOA WITO KUENZI UTAMADUNI

miz1Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
miz2Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
miz3Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
miz4Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
miz5Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama
MAELEZO
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kutambua kuenzi na kuutunza utamaduni wetu ikiwemo lugha ya Kiswahili kwani ndiyo utambulisho mkubwa wa nchi yetu. 
Mhe. Pinda ametoa wito huo leo jijini Dae es Salaam wakati akifungua kituo cha Utamaduni China nchini. Kituo hicho pekee cha utamaduni Afrika Mashariki kitatoa fursa kwa Watanzania na Wachina kubadilishana utamaduni.
Kwa kutumia kituo hichi, Watanzania wanaweza kuongeza uhusiano kwa vijana wetu hasa wenye umri mdogo kujifunza utamaduni wa China. 
“Watanzania tunatakiwa kuutambua, na kuuenzi utamaduni wetu hasa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili badala ya kuona raha kuongea lugha za wageni. Tuongee na tutumie fursa hii ya kituo cha utamaduni kuendeleza utamaduni wetu ,” amesema.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, utamaduni kwa nchi yoyote ni kila kitu ambacho mtu anakua nacho katika maisha ya kila siku.
“Ndio maana taifa lolote linalopuuzia utamaduni wake linajidhalilisha bila kujua,” amesema na kuongeza kuwa, “wenzetu wanaenzi utamaduni wao. Wana ngoma zao za asili na wamekataa kuiga tamaduni za nje hata katika ala za muziki wao zinatokana na asili yao.”
“Ala zao zinatumia Bamboo (mianzi), hata hapa tunazo kule Iringa, sisi pia tunaweza kuitumia kwa mambo mazuri kama haya badala ya kunywea pombe.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel amesema wizara yake itashirikiana na taasisi, au mtu yoyote mwenye lengo la kukuza uatmaduni wetu.
“Wizara itatoa ushirikiano kwa kila mtu au taasisi yenye lengo la kukuza utamaduni wetu kwasababu suala la utamaduni ni jukumu letu sote, kuulinda kwa nguvu zetu zote,” amesema.
Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Balozi wa China nchini Dr. Lu Youqing.

No comments: