Tuesday, December 01, 2015

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI WA CHINA, KOREA NA SUDAN

lu1Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es slaam  Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu2Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini, Dkt.Yassir  Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu3Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa   akisalimiana na balozi wa Sudan nchini,Dkt. Yassir Mohamed Ali kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu4Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu5Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kasim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu kutoka nchi za China, Sudan Kaskazini na Korea Kusini.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo mchana (Jumanne, Desemba mosi, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliwashukuru mabalozi hao kwa pongezi walizokuja kumpatia na kuahidi ushirikiano zaidi pamoja na nchi hizo.
Kwa upande wake, balozi wa China, Dk. Lu Youqing alisema Serikali itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta za uendelezaji viwanda, miundombinu, maji, afya na elimu ikiwa ni ishara kuendeleza mahusiano ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu baina ya China na Tanzania.
Alisema Tanzania imeteuliwa kuwa miongoni mwa nchi tatu ambazo zitasaidiwa na China kuendeleza viwanda na kwamba makubaliano ya mpango huo yatafikiwa kwenye mkutano wa uwekezaji baina ya China na nchi za Afrika (FOCAC – 6) unaotarajiwa kuanza Desemba 4, mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Nchi nyingine mbili zitakazonufaika na mpango huo ni Kenya na Ethiopia.
Naye Balozi wa Sudan Kaskazini. Dk. Yassir Mohamed Ali alisema nchi yake inao madaktari wengi na kwamba kumekuwa na majadiliano ya kuona ni jinsi gani wanaweza kuja kuongeza nguvu kwenye sekta ya afya. “Tuna madaktari wasiopungua 4,000 ambao wanahitimu kila mwaka na tungependa kushirikiana na Tanzania katika eneo hili,” alisema.
Naye Balozi wa Korea Kusini, Bw. Chung Il ambaye pia alitumia fursa hiyo kuja kuagana na Waziri Mkuu Majaliwa, alisema anatumaini kuona ubalozi wa Tanzania ukifunguliwa nchini mwao katika muda siyo mrefu.

No comments: