Thursday, August 06, 2015

PROF. LIPUMBA ABWAGA MANYANGA UWENYEKITI WA CUF


Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekitu wa Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.

Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.

TAARIFA KAMILI 

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani  pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu  ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA PANGANI, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI TANGA

PANGANI, TANGA – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 26, 2025, amezungumza na wananc...