Friday, August 14, 2015

NAPE NNAUYE:ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020 IKO TAYARI

1
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari,  huku akiwa ameshikilia kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Ilani hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5  ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi  kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli,  katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.
Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni 50 “Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM “.
Amefafanua  na kuongeza kuwa  “Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi”.  Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya  CCM Ofisi ndogo  Lumumba leo. 
2
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akitolea ufafanuzi mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati akizungumza nao kwenye mkutano uliofanyika CCM Lumumba jijini Dar es salaam.
3
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiionyesha ilani ya uchaguzi iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
5
Hii ndiyo Ilani yenyewe.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
7
Baadhi ya wapiga picha vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio katika mkutano huo.

No comments: