Wednesday, August 19, 2015

MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALINI YAONGEZA UFANISI KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO

AD
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw. Adolf Mapunda akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali mtandao kwa Maafisa TEHAMA, Rasilimali Watu, Utawala na Maafisa habari kutoka maeneo mbalimbali nchini jana jijini Arusha.
……………………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa – MAELEZO.
ARUSHA
Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu.
Kauli hiyo imetolewa  jana jijini Arusha  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA,Rasilimali watu,Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuondoa wizi na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu. 
Ameeleza kuwa utendaji wa Serikali na taasisi zake umerahisishwa kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

No comments: