Tuesday, August 04, 2015

MAGUFULI ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR LEO,VIFIJO NA NDEREMO VYATAWALA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi  leo agosti 4, 2015.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar. 
Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo.

 Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan wakiondoka kwa gari la wazi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu ya kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Msafara wa Mgombea Mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akipita kwenye makutano ya baabara ya Morogoro na Bibi Titi Mohammed, wakati mgombea huyo akienda kuchuua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Mwananchi akipunga mkono kufuarhia msafara wa Mgombea Mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akati ukipita kwenye makutano ya baabara ya Morogoro na Bibi Titi Mohammed, wakati mgombea huyo akienda kuchuua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

No comments: