Sunday, August 16, 2015

Kalapina wa kikosi cha mizinga achukua fomu kugombea udiwani kata ya Kinondoni kwa tiketi ACT Wazalendo!


Msanii wa muziki  wa Rap toka Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud aka Kalapina (kushoto) akipokea fomu za kugombea udiwani kata ya Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo toka kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi Bibi Ikunda Lyimo siku ya Ijumaa jioni. Kala Pina aligombea udiwani kwa tiketi ya chama cha CUF katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo alishindwa na mgombea wa CCM. 

Hapa akiwasili katika ofisi za mtendaji wa kata ya Kinondoni katika usafiri wa pikpiki.
 Akiwa ameambatana na wapambe wake waliokuwa wamepanda bodaboda
Akisalimia baadhi ya watu waliokuwa eneo la tukio.Kalapina aka nabii akihesabu pesa za kulipia fomu ya udiwani kabla hajaingia katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kata ya Kinondoni.
Washabiki wa Karama Masoud wakiamsha amsha nje ya ofisi za mtendaji.
Karama akipokea fomu za kugombea udiwani toka kwa Bibi Ikunda Lyimo, anayetazama kulia ni katibu kata tawi la Kinondoni wa ACT Bw Johnson Kapi.


Wakisikiliza kwa makini msimamimizi wa uchaguzi akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za udiwani.


Mwandishi wa gazeti la DIRA  Bi Rachel Gabagambi akimuhoji Kalapina aka Nabii baada ya kuchukua fomu.
Shangwe barabarani baada ya kuchukua fomu.

Picha na habari na Mkala Fundikira wa Keronyingi blog
Post a Comment