Wednesday, July 08, 2015

FFU WA NGOMA AFRICA BAND WAFUNGA KAZI MAMLING FESTIVAL , AUSTRIA

unnamed (3)

Mining,Austria
Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, siku ya Jumapili 5 Julai 2015 ilifanikiwa kutingisha jukwaa la Mamling Festival,lililofanyika kule Mining,Austria.kikosi kazi cha Ngoma Africa band kilipangiwa kupanda jukwaani saa 10 na dakika 30 alhasiri,lakini maporomota walisogeza muda hadi saa 12 jioni ndio bendi hiyo ilipopanda jukwaani ,muda ulisogezwa kutoka na hali jua na joto kali lililofikia nyuzi joto 38c,ambazo sio za kawaida kwa msimu wa summer barani ulaya.
Kikosi kazi kilipopanda jukwaani bila ya kuremba kilialianza kuporomosha muziki moto moto kama kawaida yake,kiasi cha kuwafanya waandaaji kutoa mwaliko tena kwa bendi hiyo kushiriki onyesho la 2016 mungu akijalia.
Ngoma Africa baada ya kumaliza kazi wamerudi katika maskani yao ya himaya Anunnaki,kule Ujerumani

No comments:

DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...