TUMUUNGE MKONO DK.MAGUFULI NDIO CHAGUO LA CCM- CATHERINE MAGIGE

SAM_4396Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha ,Catherine Magige  akizungumza jana katika mkutano wa wagombea Ubunge 12 kupitia chama cha mapinduzi waliofanya ziara ya kujinadi kwa wananchama pamoja na wananchi kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho jana katika mtaa wa kati(CCM Mkoa),ambapo hivi karibuni Catherine aliibuka ushindi wa kishindo kwa kura 409 kati ya kura 560 huku anayemfwatia akipata kura 248.
Habari picha na Pamela Mollel
SAM_4403Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha,  Catherine Magige  akisalimiana na wanachama wa chama hicho jana jijini Arusha,Aliwatoa rai kwa wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi kumuunga mkono mgombea Urais Dk.John Pombe Magufuli kwani ndio chaguo la CCM,huku pia akisisitiza wanaccm kuchagua kiongozi kwanzia ngazi ya udiwani,ubunge anayekubalika ndani ya CCMna nje ya CCM.
SAM_4391Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha, Mayasa Kimbau ambaye pia ni mratibu wa Mkoa akiteta jambo na Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha jana katika mtaa wa kati (CCM Mkoa) wakati wa ziara ya watia nia wa chama cha mapinduzi wakijitambulisha na kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama hicho katika nafasi ya Ubunge.
SAM_4404Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akifurahia jambo na mwenyekiti wa wilaya ya Arusha katika ofisi za chama cha mapinduzi jijini Arusha jana wakati watia nia ubunge 12 kupitia chama hicho walipata nafasi ya kujinadi kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
SAM_4289Mbunge viti maalum kundi la wanawake (UWT) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige  akizungumza na waandishi wa habari siku alipotangazwa kuwa mshindi.

Comments