Tuesday, July 21, 2015

KAKORE ATAJA VIPAUMBELE SABA, SAME MAGHARIBI

ka1
Mtangaza nia wa Jimbo la Same Magharibi, Ahadi Kakore akipokea fomu ua kuomba kuwania ubunge Jimbo la Same Magharibi kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Same, Mussa Matoroka hivi karibuni.
ka2
Ahadi Kakore akisaini kitabu cha wageni cha Shule ya Msingi Masandare muda mfupi baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara fupi ili kujionea hali ya shule hiyo ambayo ni moja ya shule kongwe kwa eneo hilo.Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Adelina Kiwango.
ka3
Kakore akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya Msingi Masandare iliyopo nje kidogo ya mji wa Same. Shule hiyo ipo kwenye eneo la wafugaji. 
………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, SAME
MTANGAZA nia kwenye Jimbo la Same Magharibi, Ahadi Kakore asema kuwa iwapo atapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kunakuwa na mabadiliko ya kweli na yaharaka katika maeneo saba tofauti.
Akizungumza mjini Same kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Same, Kakore ambaye ni mwandishi wa habari za michezo amesema kuwa nia yake ni kuona jimbo hilo linafanana na majimbo mengine ya mkoa wa Kilimanjaro ambayo yamepiga hatua katika ameneo mengi tofauti.
Alisema miongoni mwa maeneo ambayo atayasimamia kwa nguvu punde atajkapoingia bungeni ni pamoja na Miundombinu ya barabara, Afya, Maji, Usalama wa raia, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kisasa, michezo sanaa na ukuzaji wa vipaji kulingana na dunia ya sasa.
“Nipo tayari kuwatumikia wana Same Magharibi, naamini huu ni wakati wa vijana, mimi ndiye mtu ninayefahamu vyema matatizo ya jimbo letu ambalo kiukweli bado lipo nyuma kwenye maneoe mengi.
“Iwapo nikipata ridhaa ya kuwa mbunge wa Same Magharibi nitahakikisha kuwa maeneo yaliyokwama na yaliyokuwa wanaonekana ni miujiza kutendeka itakuwa kweli kwani kila jambo linawezekana.
“Naamini katika watu ndiyo maana nasisitiza kuwa watu waliopo ninashirikiana nao kulivusha jimbo letu kama Mussa aliovyowavusha wana wa Israel kutoka Misri kwenda nchi ya Ahadi, mimi nipo kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema Kakore.
Aidha Kakore amesema kwamba katika suyala la elimu litaenda sambamba na maendeleo ya michezo na ukuzaji wa vipaji ambapo yupo kwenye mazungumzo na mamlaka husika ili kuweza kuifanya Shile ya Msingi Masandare iwe moja ya shule za kukuza vipaji jambo nlitakalosaidia pia kupunguza tatizo la utoro hasa kwa jamii za wafugaji.
Jimbo la Same Magharibi kwa sasa linasikiliwa na Mathayo David Mathayo ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi kwenye serikali ya awamu ya nne ambayo inamaliza muda wake mwaka huu.
 Katika hatua nyingine Kakore alifanya ziara kwenye Shule ya Masandare na kujionea hali ya mazingira ya shule hiyo huku shule hiyo kongwe ikiwa inakabiliwa na tatizo la usalama kwa kukosa uzio, ukisefu wa vifaa vya michezo na kumalizia jembo la maktaba ambapo aliahidi kuyashughulikia ndani ya muda mfupi ujao.
Tayari vifaa vya michezo vinatarajiwa kukabishiwa kwa uongozi wa shule hiyo, ndani ya muda mfupi ujao kutoka sasa huku suala la uzio na jengo la maktaba ya shule yakipatiwa ufumbuzi baada ya Oktoba mwaka huu.

No comments: