SAFARI YA KUJIMBULISHA YA MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI KUTOKA CHATO MPAKA DODOMA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa
chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie
wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa
wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia
wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni
mkoa wa Singida.
 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli(kulia) akisalimiana na
aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini Dk. Hamisi Kigwangala
 Hussein Bashe ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Nzega Mjini
akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli
mjini Nzega. 
 Wananchi wa Nzega wakishangilia mara baada ya kumisikiliza  Mgombea Urais wa
chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  alipomaliza kuwasalimia
na kuwashukuru kwa namna walivyojitokeza kumtia moyo,nje ya  za CCM
Nzega.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Nzega
kwenye mkutano uliofanyika nje ya ofisi ya CCM wilayani hapo, ambapo
aliwaambia Wananchi kuwa amefarijika na mapokezi mazuri na amewaahidi
kurudi tena wakati wa kampeni zitakapoanza.
.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya  wageni
Ofisi za CCM ndani ya mji wa Manyoni  mkoani Singida alipokuwa akipita
kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha
kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya
barabara.
 Wananchi wa Igunga wakiwa na Bango lao wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia
CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili maeneno hayo kuwashukuru
na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea
jijini Dar kwa njia ya barabara.
Wananchi wa Ikungi wakiwa wamelizunguka gari la Mgombea Urais wa chama cha
Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka
awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiondoka nzega huku
shangwe zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki mara baada ya kuwashukuru
kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea
jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.
 Wananchi wa Igunga wakimshangila  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe
Magufuli mara baada ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,na
pia alijitambulisha kwao.Dkt Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa ana
mambo ya kuwaambia lakini kwa sasa anapita kujitambulisha kwao,kwa
sababu wakati wa kampeni bado haujafika,lakini ukifika basi atarejea
tena kuzungumna nao kinagaubaga. 

Comments