Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Johansen Kahatano akifungua rasmi warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Gianluca Azzon Mwakilishi wa EU Nchini Tanzania akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Tom Bishop kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMEND akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na Jumuiya ya umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku.
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Kibuda Chalila Mwandishi mwandamizi wa Michuzi Media.
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mwandishi wa habari wa magazeti ya serikali TSN Bi. Regina Kumba.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika warsha hiyo
…………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa suala la usalama barabarani ni ni jukumu la kikosi cha usalama barabarani hali ambayo jamii imejengeka na utamaduni huo na kusahau suala hilo ni jamii nzima katika mapambano ya kupunguza ajali za barabarani.
Hayo ameyasema leo Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano wakati wa mafunzo kwa waandishi habari juu ya kuhabarisha jamii katika suala la usalama barabarani iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU)
Kahatano amesema kuwa kikosi cha usalama barabarani kimekuwa kikitoa elimu juu ya usalama barabarani kwa wananchi pamoja na madereva katika kuzingatia sheria zilizowekwa katika kuondokana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.
Amesema jamii ikipata mwamko wa katika kutambua sheria za usalama barabarani kuna uwezekano wa kuondokana na ajali ambazo zinapoteza watu pamoja na kuacha watu wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.
“Kikosi cha usalama barabani pekee yake hakiwezi ni wakati umefika kwa jamii kuweka suala hili kwenye vichwa vyao kuwa wanamchango katika wa kusukuma gurudumu katika kupambana na ajali katika sehemu zao”amesema Kahatano.
Katika kuhamasisha masuala ya Usalama Barabarani ,Mwandishi wa Citizeni Mkinga Mkinga amesema ni wakati umefika kwa waandishi kutambua umuhimu wetu wa kutoa taarifa za kuelimisha wananchi juu ya usalama barabarani.
Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika mashule ili kuweza kuondokana na ajali za wanafunzi katika maeneo ya karibu na barabara.
Comments