NANI KUAGA SHINDANO LA TMT 2015 #MPAKAKIELEWEKE WIKI HII?

 Baadhi ya washiriki wakiwa kazini katika kutengeneza filamu mfupi
 Baadhi ya washiriki wakiwa makini huku sura zao zikiwa na majonzi na wasiwasi juu ya washiriki gani wanaooaga shindano kwa wiki hii.
 Baadhi ya watazamaji waliojitokeza katika kushuhudia mtanange wa washiriki wanaaga mashindano katika wiki hii na kushuhudia wanaoingia katika jua la utosi
 Walimu wa Washiriki wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke kutoka Kushoto Ni Mwl Issa na Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia kazi ya wanafunzi wao katika kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke
 Majaji wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia show ya washiriki wa TMT waliobahatika kuendelea na shindano hilo mara baada ya washiriki wengine kuaga mashindano hayo kutokana na kura kutotosha.
 Mahosti wa Kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia kazi yao wakati wa kipindi cha TMT kinachorushwa kila jumapili saa tatu na nusu usiku kupitia kituo cha ITV
Baadhi ya washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kutaja waliongia hatua ya jua la utosi.

Na Josephat Lukaza.

Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke limeingia hatua nyingine tena mara baada ya washiriki wengine kuaga shindano hilo . Katika hatua hiyo ya mchujo hali imezidi kuwa ngumu kwa washiriki kutokana na shindano kuwa gumu kwao kila wiki. Mpaka sasa jumla ya washiriki wanne wameshaaga shindano hilo huku mchuano ukiwa mkali kwa washiriki waliobakia.

Ili kuweza kumbakiza mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumnusuru na kuaga shindano ambalo limejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kutokana na ubora wake na uwajibikaji na ubunifu wa shindano hilo

Jinsi ya kumpigia kura mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika ujumbe mfupi wa Maneno TMT ikifuatiwa na namba ya mshiriki halafu tuma kwenda namba 0784 36 77 38.

Kufahamu ni nani na nani wameaga shindano hili kwa wiki hii basi usikose kufuatilia kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke kupitia kituo cha runinga cha ITV kila siku ya Jumapili saa tatu na nusu usiku.

Shindano la TMT limepigwa Tafu na I-View Studio, Precision Air, Global Publishers, Paisha, Cam Gas, Radio One na ITV pamoja na Pepsi

Comments